Saturday, June 15, 2013

Afa kwa kunywa komoni

MWANAKIJIJI wa Matandalani, Ngusa Solea (32) amefariki dunia baada ya kunywa pombe aina ya komoni inayosadikiwa kuwa na sumu
.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi, Dhahiri Kidavashari alisema kifo hicho kilitokea juzi saa tatu asubuhi kwenye kijiji hicho kilichopo kwenye Tarafa ya Nsimbo.

Kwa mujibu wa kamanda huyo, mwili wa marehemu ulikutwa nje ya nyumba inayojengwa jirani na nyumba ya Anisety Matongo ukitokwa damu puani.

“Inaelezwa kwamba marehemu alikuwa akinywa pombe hiyo nyumbani kwa Matongo na haikufahamika aliondoka saa ngapi.
“Chanzo cha kifo hicho kinadhaniwa  kuwa ni pombe yenye sumu,” alisema kamanda huyo na kuongeza hakuna aliyekamatwa kuhusiana na kifo hicho. 

No comments:

Post a Comment