Rais wa Marekani Bw. Baraka Obama na Mkewe wanatarajia kufanya ziara ya nchi tatu barani Afrika itakayojumuisha nchi za Senegal, Afrika ya Kusini na Tanzania, Kuanzia tarehe 26 Juni hadi tarehe 3 Julai.
Katika ziara yake hiyo, Rais atawekea mkazo umuhimu
ambao Marekani inauweka katika ushirikiano wetu wa kina na unaoendelea kuimarika
na nchi za Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara kupitia mipango mbalimbali ikiwemo
ile ya kuimarisha ukuaji wa uchumi, uwekezaji na biashara, uimarishaji wa
taasisi za kidemokrasia na uwekezaji katika kizazi kipya cha viongozi wa
Kiafrika.
Rais atakutana na viongozi mbalimbali wa kiserikali,
sekta binafsi na jumuiya huru ya kiraia ikiwemo vijana ili kujadili ubia wetu wa
kimkakati katika ushirikano wetu rasmi na masuala mengine ya
kimataifa.
No comments:
Post a Comment