Thursday, June 6, 2013

.Uingereza yakubali kuwafidia Mau Mau

Uingereza imekubali kuwalipa fidia na kuwaomba msahama walioteswa wakati wa ukoloni wa Muingereza Kenya
Serikali ya Uingereza imetangaza kuwa itawalipa fidia ya dola milioni thelathini manusura wa harakati za ukombozi wa Uhuru wa Kenya Mau Mau.
Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza William Hague ametangaza kuwa serikali yake itawalipa wale wote walioteswa na askari wa ukoloni katika miaka ya 1950.
Waliokuwa wanachama wa vuguvugu hilo waliwasilisha kesi mahakamani kwa mateso na dhuluma walizodai kutendewa na uliokuwa utawala wa ukoloni miaka ya 50.Huenda pia Uingereza itatangaza fidia.
Zaidi ya wakenya 5,000, waliteswa baadhi wakinyanyaswa na waliokuwa wakoloni wa Uingereza.
Uingereza ilipigana vita vikali dhidi ya Mau Mau, waliokuwa wanadai ardhi na kuondoka kwa utawala wa kikoloni.
Baadhi ya waliokuwa wanachama wa Mau Mau
Manusura wa vita hivyo wamekuwa wakiidai Uingereza kuwalipa fidia kwa miaka mingi.
BBC ina habari kuwa bwana Hague atawaomba radhi waathiriwa wa vita vya Mau Mau, wakati akitangaza kiwango cha pesa watakazotoa kama fidia kwao.
Serikali ya Uingereza awali ilikuwa imesema kuwa madai yote ya vitedno walivyofanya wakoloni ni juu ya serikali ya Kenya tangu kuipa uhuru mwaka 1963 na kuwa kwa sasa haiwezi kutakiwa kulipa.
Lakini mwaka 2011, mahakama iliamuru kuwa, wanaodai fidia, Paulo Muoka Nzili, Wambuga Wa Nyingi na Jane Muthoni Mara, walikuwa na haki ya kudai fidia kutoka kwa Uingereza .
Mawakili wao wanasema kuwa Nzili alihasiwa , huku Bwana Nyingi akichapwa vibaya wakati Bi Mara akiteswa kimapenzi katika kambi za mateso ambako waliokuwa wanapinga ukoloni walikuwa wakifungwa.
Baada ya uamuzi wa kesi hiyo, ilirejeshwa katika mahakama kuu ili kuamua pesa watakazolipwa na ofisi ya jumuiya ya madola.
Mahakam kuu Uingereza iliamua kuwa walalmishi walipaswa kutendwa haki
Duru zinasema kuwa serikali ilikumbwa na wakati mgumu kupata mashahidi na stakabadhi muhimu kuweza kuelezea ukweli katika kesi hiyo.
Lakini Oktoba mwaka jana, mahakama iliamua kuwa waathiriwa waliowasilisha kesi hiyo mahakamani walikuwa na haki ya kufidiwa kwani walikuwa na kesi nzito dhidi ya serikali ya Uingereza.
Watatu hao walikuwa wamesema kuwa wangekubali wahusika wa kesi kuafikiana nje ya mahakama lakini pia walikuwa wanataka kufuata sheria kwani waliona wangepata haki katika mahakama.....

1 comment: